Audio Mp3
Tuesday, February 6, 2018
CCM yazungumzia kutekwa diwani wa CHADEMA
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa CCM hakihusiki kivyovyote vile na kutekwa kwa mgombea wa Udiwani wa CHADEMA Kata ya Buhaganza , Nelson Athanas ambaye alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui.
Tibaijuka amedai kuwa kuwekuwepo na tetesi kuwa chama chake kimehusika na kitendo hicho cha kinyama na kudai kuwa hilo ni lengo la kutaka kuvuruga uchaguzi huo hivyo amesisitiza kuwa chama chake hakihusiki na unyama huo.
"Kamati ya siasa ya wilaya ya Muleba imeamua kuwajulisha wananchi rasmi na wapiga kura wa Kata ya Buhaganza na Umma wa Watanzania kiumjula kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiusiki kwa lolote lile na tuhuma hizo zinazoongozwa kwake na viongozi wake kwa nia mbaya ya kuwachafua na kukichafua chama na kuvuruga uchaguzi baada ya kuzidiwa.
"CCM kimejitayarisha vyema kwa ushindani na kinaamini mgombea wake Bi. Jenitha Tibihenda anatosha hivyo hakuna haja ya kumteka mshindani wake yoyote yule tupo imara" alisema Tibaijuka
Aidha Tibaijuka alivitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa tukio hilo kwa haraka ili watu waliotenda tukio hilo ovu waweze kupatikana kwa haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mgombea wa udiwani Kata ya Buhangaza, Muleba (CHADEMA), Athanasio Makoti aliyekuwa amepotea tangu Februari 2, 2018 alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui, CHADEMA imesema alitupwa barabarani maeneo ya Hospitali ya Kagondo na sasa aendelea kupatiwa matibabu.
Dk Slaa: Sijaja Tanzania kuapishwa kuwa balozi
Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa amesema amekuja nchini kwa ajili ya kushughulikia usajili wa Hospitali ya CCBRT.
Katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema, ametoa kauli hiyo leo Februari 6, 2018 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Clouds.
“Familia yangu nimeiacha Canada, wengine wanajua, sikuja kwa sababu ya ubalozi. Mimi ni mwenyekiti wa CCBRT ndicho kimenileta na wengine mnafahamu katika nchi yetu mengi yanafanyika,” amesema.
Novemba 23 mwaka jana, Rais John Magufuli alimteua Dk Slaa kuwa balozi, lakini mpaka sasa hajaapishwa na kupangiwa kituo cha kazi.
Dk Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia muungano wa Ukawa.
Alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwamo Lowassa.
Januari 29, 2018, Dk Slaa alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu Dar es Salaam na kumshukuru kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.
Katika kipindi hicho, Dk Slaa ameulizwa kama amekuja kula kiapo na kupangiwa kituo cha kazi, lakini amepinga jambo hilo na kubainisha kuwa amekuja kushughulikia usajili wa hospitali hiyo kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa bodi.
Amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria, CCBRT inatakiwa kujiandikisha upya vinginevyo itafutwa.
Kuhusu taarifa kuwa ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za nyumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, amesema: “Hizo ni propanganda nisingependa kuzizungumza lakini Supermarket inayozungumzwa si kama mnavyofikiri ni kubwa.
“Kitu kikubwa tunatofautiana katika mtazamo, fikra tunavyofanya vitu vyetu. Canada haina mwenyewe kuna raia wa kutoka kila nchi. Sisi hapa tunasema hapa kazi tu lakini kule ni maisha. Unakuta waziri anatoka ofisini kwake anakwenda kufanya kazi nyingine, baadaye anatoka na kwenda kufanya nyingine. Kufanya kazi tatu ni kawaida.”
Ametolea mfano ufanyaji kazi wa Canada na Tanzania amesema baadhi ya Watanzania huingia ofisini na kusoma magazeti, au kutumia simu kufanya biashara zao.
“Canada utaingia ofisini na simu au ipad lakini utaiacha getini na matokeo yake nchi ile ni matajiri. Watu ni matajiri kila mtu ana utambuliso wa maisha mazuri ni kwa sababu wanafanya kazi na huduma zote ziko vizuri,” amesema.
Kuhusu kufunga ndoa amesema: “Siasa za Tanzania zilichangia mimi kutokufunga ndoa kwa kipindi chote lakini Februari 2016 kule Canada nilifunga ndoa (na Josephine Mushumbusi), ile si ndoa kwani tulishakaa, kanisa ilichokuja kufanya ni kuhalalisha tu.”
Mahakama yaagiza Nabii Titto apime upya akili
MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kujiridhisha kama ana matatizo ya akili.
Licha ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza mahakama.
Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa kutokana na mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na alifanya tukio hilo kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa vinamwamuru akate, mahakama itabidi ipate vielelezo ambavyo vitathibitisha anachokisema.
Karayemaha alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu, hivyo hana hatia.
“Mshitakiwa anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbli ikiwemo ya Maweni. Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake vyote viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.
Pia alisema kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya akili kwa mujibu wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa, atakuwa na kesi ya kujibu.
“Kutokana na hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la dhamana tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini kama itabainika kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo vitakavyoletwa pamoja na vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana litafanyiwa kazi,"alisema.
Hata hivyo alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa Februari 19, mwaka huu.
Wakati kesi itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.
Nabii Tito anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata


