Audio Mp3
Tuesday, October 15, 2019
Thursday, January 24, 2019
Matokeo Kidato Cha Nne 2018-2019
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
CSEE 2018 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES
kupata matokeo ya kidato cha nne bofya link hapa chini
https://matokeo.necta.go.tz/csee/csee.htm
Sunday, January 13, 2019
Chikuna ft Mbosso - Pieces Lyrics
Read more at: https://afrikalyrics.com/en/chikune-pieces-remix-lyrics
Read more at: https://afrikalyrics.com/en/chikune-pieces-remix-lyrics
Friday, January 4, 2019
MATOKEO YA DARASA LA NNE 2018
http://41.59.85.99/results/2018/sfna/sfna.htm
Link ya Pili
https://www.necta.go.tz/
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018
https://www.tanzania.go.tz/FTNA-2018/index.htm
Link ya Pili
https://www.necta.go.tz/
Thursday, May 31, 2018
ALAMA ZA MWANAMKE ANAYEKUHITAJI KIMAPENZI
May 31, 2018 12:40 PM
KARIBU kila kitu huwa na dalili zake. Mvua ina dalili, homa ina dalili, hata kwa mujibu wa mafundisho ya dini siku ya mwisho pia ina dalili zake. Kupitia hizo dalili, ndiyo hasa huwa tunajua uwepo au kutokuwapo kwa kitu.
Japo si mara zote mawingu yakitanda huwa mvua inanyesha, ila huwa mara nyingi yakitanda mvua hunyesha. Kilichokusudiwa hapa ni kwamba, kuna mienendo na mambo hutokea kutoa ufahamu wa kitu fulani.
Wanawake ni tofauti sana na wanaume. Matendo mengi yanayofanywa na wanaume ni wanawake wachache sana huweza kufanya, tena pengine hufanya chini ya viwango na mbinu husika zinazotumiwa na wanaume.
Yapo matendo mengi kama kukimbia, kupigana, hata jinsi wanavyowaza na kuamua. Ila hapa najadili kuhusu mapenzi.
Si mara zote mwanamke huwa anamwambia mwanamume hisia zake moja kwa moja, kama ambavyo wanaume wamekuwa wakifanya. Ndiyo kuna wanawake wana uwezo huo, ila ni wangapi? Ni wachache sana.
Katika jamii jukumu la kueleza hisia za mapenzi linaonekana hasa ni la kiume. Wanawake wamebaki kuwa wasikilizaji tu au kama akiwa naye kapenda kweli hubaki kuonesha hali hiyo kupitia ishara.
Wanawake wengi hufanya hivi badala ya kusema nini wanajihisi kwa kina fulani. Unamjua mwanamke anayekupenda wewe? Hata kama hajasema akiwa na ishara zifuatazao huyo atakuwa na hali ya hisia fulani za upendo na wewe.
(i)Atapenda kuongea na wewe, kila anapopata nafasi atapenda kuwa na wewe karibu mkiongea. Atakuwa makini na kufanya kila analoweza kuona kuwa anaheshimu mazungumzo yako na uwepo wako. Inaweza kuwa huwa anaongea na watu wengi, ila uongeaji wake utakuwa tofauti sana na akiwa na wewe. Kwako atakuwa na heshima zaidi na utulivu zaidi, tena akiwa ana ujasiri wakati mwingine atapenda kugusana na wewe muwapo katika mazungumzo yenu. Hata kama hakuna ulazima anaweza kugusisha bega lake kwako au hata kugongesha viganya. Yote anafanya katika hali ya kuipa furaha nafsi yake pamoja na kuonesha ni kwa namna gani kwako alivyo huru.
Mwanamke huwa muoga sana kugusana na mwanamume, ila woga huo hutoweka akiwa na hisia fulani nzuri juu yako. Hata kama ukimgusa bahati mbaya maeneo kama ya maziwa na hata kwenye makalio hawezi kukutukana wala kujisikia vibaya kama akifanyiwa na mtu asiye na hisia naye.
(ii) Atakuwa na nidhamu kwako, ndiyo, anaweza kuwa mtu wa nidhamu siku zote. Ila hapa kwako itakuwa zaidi.
kwa kipindi chote anachokutana na wewe atahakikisha anaonesha hali ya nidhamu kwako na unyenyekevu. Kwake hali hii itakuwa na tafsiri mbili; kwanza anataka kuonesha kwamba wewe ni mtu muhimu sana kwake ila pili atataka uone raha na furaha kuongea na yeye.
Wakati mwingine nidhamu yake huwa kama pia imechangiwa na aina fulani ya woga, ila hufanya hivi katika namna ile ile ya kukuonesha ubora na hadhi katika moyo wako.
(iii) Atafanya kitu kwa ajili yako, hata mkiwa mmekutana pamoja halafu wewe ukaonesha una shida na kitu fulani, aidha nguo au hata kitabu, yeye kama pesa anayo atataka kukununulia.
Jambo hili kwake huwa ni katika hali ya kuweka alama katika maisha yako na kuonesha ni kwa kiasi gani ulivyo na umuhimu katika maisha yake. Hata nauli mkiwa pamoja atataka kukulipia ikiwa tu ana pesa za kutosha.
Atajitahidi kwa kila hali kukuonesha yuko tayari kwa ajili ya kukupa furaha na kuonesha umuhimu wako katika maisha yake.
(iv) Kukupa zawadi, haijalishi ni ya gharama kiasi gani, ila atataka kukupa zawadi ikipatikana nafasi ya kufanya hivyo.
Zawadi ni kipimo cha thamani na kumkumbuka mtu. Yeye atafanya hivi katika hali hiyo na ili umfikirie zaidi. Tena akiwa mjanja zaidi anaweza kukupa zawadi zenye uashiriao wa mapenzi na kumbukumbu.
Kwa mfano anaweza kukununulia saa au kitu chenye maandishi yenye kujenga hali ya mapenzi na kuonesha dhamira yake kwako. Hapa wengi huwa ni waoga kutoa zawadi za maua au kadi, japo kuna wengine wana uwezo wa kufanya hivyo.
Woga wao unakuja kutokana na zawadi husika kuwa wazi sana kuonesha dhamira zao.
(v) Kutaka kujua mengi kuhusiana na familia yako, ili kuonesha ni kwa namna gani anahitaji nafasi katika maisha yako, atataka kujua mambo unayoyapenda na kujua vitu muhimu katika familia yako.
Atataka kujua wewe ni wa ngapi kuzaliwa, kabila lako na asili yako kwa ujumla. Pia atataka kujua chakula na mavazi unayopenda, aina ya familia na mwanamke unayetaka kuwa naye katika maisha yako.
Kwa mwanamke mjanja yeye atakubana sana katika maswali ya namna hii, ila nawe ukitaka kumpa maswali atakujibu kwa namna ya majibu yako kwake yalivyo.
Kwa mfano; unaweza kusema unapenda mwanamke wa aina Fulani, ila kama yeye tayari kakuuuliza na umemjibu swali la mwanamke unayempenda atakujibu kwa mujibu wa jibu lako. Hata kama ataongeza kitu ila si katika namna ya kutoa maana halisi ya kitu ulichoongea.
(vi) Atata kuishi kwa namna unavyopenda, baada ya kujua wewe ni mtu wa aina gani kupitia maswali na mfumo mzima wa maisha yako, atataka kuishi namna unavyopenda ili uweze kuvutiwa naye. Kama atajua hupendi mwanamke mapepe hata siku moja hawezi kujichetua kwa kuamini kwa kufanya hivyo atakuwa anakufukuza.
Akijua hupendi mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume hata kama alikuwa nao atafanya kila njia kuachana nao. Yote atayafanya katika hali na namna ya kukuonesha kuwa yeye ni mtu anayekufaa katika maisha yako.
(vii) Atakuwa na huruma zaidi kwako, akihisi una matatizo au unapitia katika hali ngumu ya kimawazo atataka kuwa karibu zaidi na wewe pamoja na kukupa maneno ya kukutia nguvu na imani zaidi. Hata siku moja hawezi kukuacha ukiwa unataabika kifikra na kuumia peke yako, katika kila namna atakayoweza atataka kuonesha ni kwa kiwango gani anaweza kukufuta machozi na kujenga tena tabasamu katika sura yako.
(viii) Atazungumzia mipango yake ya mbele kwako, ili kukuvuta zaidi kwake ataweza kukueleza nini mipango yake ya baadaye na namna gani alivyo na dhamira ya kweli katika kufikia ndoto zake.
Atafanya hivyo kukufanya ujue yeye ni mtu mwafaka na bora sana katika maisha yako. Atataka ujue unapoingia naye katika uhusiano basi, utakuwa na mtu mwafaka katika maisha yako ambaye atakufanya uyaone maisha mepesi kwa usaidizi wake.
(ix) Atakusikiliza kwa makini na kutekeleza unayopenda, kwa ajili ya kukuvuta kwake atakuwa makini katika kukusikiliza na kufanya yale unayopenda kufanyiwa au unayotamani kufanyiwa.
Hata bila kumtaka afanye yeye atafanya kwa umakini huku akiwa makini kuona mwitikio wako katika suala husika, akiona umefurahia atafanya hivyo kadri atakavyopata wasaa wa kufanya.
UKAWA wapigwa chenga
BUNGE jana 'liliupiga chenga ya mwili' Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kupitisha makadirio ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.....
.....kwa mwaka ujao wa fedha bila uwapo wa mbunge hata mmoja wa upande huo, ikiwamo chama kikuu cha upinzani nchini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Katika kikao cha jana cha Bunge kilichofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa saba mchana, hapakuwa na mbunge hata mmoja wa Chadema bungeni kutokana na kile kilichoelezwa na uongozi wa chama hicho kuwa wabunge wake wengi walikuwa mkoani Kigoma kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, Kuasuku Bilago.
Mwili wa mbunge huyo aliyefariki dunia Jumamosi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) uliagwa juzi na wabunge jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa ajili ya mazishi.
Huku ratiba ya vikao vya Bunge la Bajeti ikionyesha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yalipaswa kujadiliwa kwa siku tatu, Bunge jana lilitumia muda wa takribani saa nne kuyajadili na kuyapitisha huku viti vinavyokaliwa na wabunge wa Chadema vikiwa tupu.
Ratiba ya vikao vya Bunge la Bajeti inaonyesha kuwa makadirio ya bajeti ya wizara hiyo yalipaswa kujadiliwa bungeni kwa siku tatu kuanzia Jumatatu, lakini hayakuwasilishwa bungeni siku hiyo kutokana na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge kufuatia kifo cha Bilago.
Juzi, Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, aliwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake lakini hayakujadiliwa na Bunge kwa kuwa kulikuwa na shughuli ya kuaga mwili wa Bilango kwenye Viwanja vya Bunge.
Wakati wa kuipitisha bajeti hiyo jana, hakuna mbunge hata mmoja wa vyama vilivyokuwa na wabunge bungeni jana aliyewasilisha hoja ya kuzuia mshahara wa waziri, hivyo bajeti hiyo ya Sh. bilioni 65 kupita bila kupingwa.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, aliyekuwa anaongoza kikao hicho, alisema kukosekana kwa mbunge wa kuipinga bajeti hiyo ni matokeo ya uchapakazi wa Waziri Lukuvi na wasaidizi wake.
Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha (2017/18) pia ilipita bila kupingwa na mbunge yeyote wakati wa Bunge la Bajeti la mwaka jana huku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akiwataka mawaziri wengine kuiga utendaji wa Lukuvi.
'TUPO KIGOMA'
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika, alipotafutwa kuzungumzia kutokuwapo kwa wabunge wote wa chama chake bungeni jana alisema: "Kimsingi wabunge wengi tupo huku Kigoma na wachache wana udhuru."
Mbunge wa Kibamba huyo alibainisha kuwa wabunge wa chama chake watarejea bungeni kushiriki vikao vya Bunge baada ya mazishi.
Sunday, February 25, 2018
Wednesday, February 21, 2018
Walimu wa sekondari kufundisha Shule za msingi Serikali yatoa tamko
Serikali imesema mwalimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi si kushushwa cheo na wala si jambo la ajabu.
Taarifa ya mkuu wa kitengo cha mawasiliano Ofisi ya Rais (Utumishi), Florence Lawrence imesema Serikali kuwapangia baadhi ya walimu wa sekondari kufundisha shule za msingi ni moja ya hatua za kuongeza ufanisi na kuleta mgawanyo sawa wa walimu katika shule hizo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro amekaririwa katika taarifa hiyo iliyotolewa leo Februari 20,2018 akisema hatua hiyo haimaanishi kuwa walimu wanaotoka katika shule ya sekondari kwenda kufundisha msingi wameshushwa cheo.
Dk Ndumbaro ametoa ufafanuzi huo katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Amesema lengo la Serikali ni kuondoa upungufu wa walimu katika shule za msingi na kuimarisha utoaji wa elimu.
Katibu mkuu ameainisha kuwa sifa za kufundisha na kiwango cha elimu zinaendana na mabadiliko yanayotokea duniani, hivyo mwalimu mwenye elimu ya kiwango cha Shahada ya kwanza kufundisha shule ya msingi isionekane ni jambo la ajabu.
Dk Ndumbaro amewaambia watumishi wa umma kuwa, maendeleo katika sekta yoyote, ikiwamo ya elimu yanakuja na mabadiliko hivyo wayapokee na kufanya kazi ili kufikia lengo.