Audio Mp3

audio song

Monday, June 12, 2017

ACACIA wapinga vikali matokeo ya kamati ya pili ya Rais

ACACIA wapinga vikali matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia 

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

1 comment:

  1. Testimony on how i got my LOAN from fundingloanplc@yahoo.com

    I'm Isabella Tyson from 1910 N Halsted St Unit 3, Chicago IL60614 USA,, i have been searching for a genuine loan company for the past few months and all i got was bunch of scams who made me to trust them and at the end of the day took my money without giving anything in return, all hope was lost i got confused and frustrated, i find it very difficult to feed my family and vowed never to have anything to do with loan companies on net and went to seek of assistance from a very good friend which i explained all my experience regarding online companies with and said he can help me that he knows of a Godsent and well known company called FUNDING CIRCLE PLC, he stated he just got a loan from them although i was still very unsure about this company due to my past experience but i decided to give it a try and did as i was directed by my friend and applied, i never believed but i tried and to my greatest surprise i received my loan in my bank account within 24 hours, i could not believe that i would stand on my feet financially again. I’m glad I took the risk and applied for the loan and today i'm thanking God that such loan companies still exist and promise to share the good news to people who are in need of financial assistance because the rate of scams on net is getting very serious and i don't want people to fall victim when we still have genuine and Godsent lenders.. You can contact this Godsent company using the information as stated and be a partaker of this great testimony.. Email: fundingloanplc@yahoo.com OR Call/Text +14067326622 thanks



    ReplyDelete